Duration 10:6

AMRI 10 ZA MUNGU/MAKANISA YATOFAUTIANA/KUABUDU SANAMU

13 451 watched
0
170
Published 24 Apr 2021

#Amri10#Musa#Sanamu#Farao Amri kumi ni Nakala ya Tabia ya Mungu na ni kanuni ya Ufalme wake. Amri kumi zinafunua Upendo, Haki, wema na Utakatifu wa Mungu. Mtume Paulo akielezea asili ya zile Amri kumi aliandika hivi: “Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria. [War13:8-10]. Na tena Mtume Paulo anaandika hivi: “Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema. [Warumi7:12]. Amri kumi za Mungu zilikuwepo tangu Uumbwaji wa Wanadamu, na ni mafunuo ya Sheria ile ya upendo iliyokuwepo tangu milele Mbinguni ikiwaongoza Malaika watakatifu mbinguni. Hapo Mwanzo Mungu alipomuumba Mwanadamu wa kwanza, Aliandika sheria yake Mioyoni mwao. Waliumbwa na asili inayopatana na Sheria zake zilizoandikwa Mioyoni kwao na walifanana na Mungu kitabia. Baada ya Adam na Eva kumwasi Mungu asili yao ikabadilika ikawa asili ya Kumwasi Mungu kuliko kumpenda na Kumtii. Ingawa toka kizazi hadi kizazi kwa kiasi kikubwa Wanadamu walimwacha Mungu na kuabudu viumbe vya Asili badala ya Muumba, bado sheria za Mungu zilibaki ndani ya mioyo yao zikiwashuhudia kuwa wayatendayo ni maovu. Biblia yasema hivi: “Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea; [Warumi2:14-15]

Category

Show more

Comments - 17